Klabu Real Madrid imethibitisha kuvunja mkataba na kiungo Eden Hazard kwa makubaliano ya pande zote ambapo nyota huyo raia wa Ubelgiji atakuwa huru kuanzia Juni 30, 2023.
Mkataba wa Hazard (32) ulikuwa utamatike Juni 2024 lakini klabu hiyo imeamua kuukatisha mwaka moja kabla ikiwa ni miaka minne tangu ajiunge na klabu hiyo kwa ada ya uhamisho ya euro milioni 150 kutoka Chelsea.
Hazard amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara yaliyomfanya ashindwe kuonesha kiwango kilichoifanya Real Madrid kutoa kiasi hicho cha pesa kuinasa saini yake.
Akiwa Real Madrid kwa misimu minne Hazard ameshinda mataji 8 ambayo ni Ligi ya Mabingwa Ulaya ×1, Kombe la Dunia la Klabu ×1, UEFA Super Super Cup ×1, Mataji 2 ya LaLiga, Copa del Rey ×1 na Super Cups ya Uhispania ×2.
#udakuTanzania
0 Maoni