MWANAUME AKUTWA NA UJAUZITO ZANZIBAR, KIPIMO CHABAINI.
Kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka 2021/2022 imebainika kuwepo kwa mazingira yasiyofaa ya kuhifadhia dawa na vifaa tiba katika baadhi ya Hosptali na vituo vya afya, hali iliyopelekea baadhi ya dawa pamoja na vitendanishi kuharibika kabla ya muda wake na kusababisha kutoa majibu yasiyo sahihi.
Hayo yameelezwa Ikulu Zanzibar na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar Dkt.Othman Abbas Ali, ambapo amesema baadhi ya vituo vya afya na hospitali vililazimika kusitisha vipimo vya upimaji wa mkojo kwa ajili ya ujauzito (UPT) baada ya kuona vinatoa majibu tofauti ikiwa ni pamoja na kipimo hicho kuonyesha mwanaume ana ujauzito.
"Mhe. Rais Dkt.Mwinyi, tumekwenda vituo vya afya ukienda pale ukiwa Mjamzito tumbo kubwa unaonekana si Mjamzito na ukiwa si Mjamzito ukienda unaonekana ni Mjamzito, sitaki kuvitaja hapa"
"Lakini pia kulifanyika kipimo cha mkojo kilibaini pia mwanaume ni Mjamzito"- Dkt. Othman Ali, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar alipokuwa akiwasilisha taarifa za ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo Juni 3, 2023.
Nini Maoni yako
Endelea kufatilia blog yetu kwa Habari mbali mbali
0 Maoni