Ticker

6/recent/ticker-posts

Adsterra ad

JINSI YA KUPIKA DONATI ZA HAMIRA

JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA DONATI ZA HAMIRA. Vipimo Unga – 1/2kg Sukari robo Mayai 5 Siagi - 4 Vijiko vya chakula Hamira 1 Kijiko cha chakula Baking Powder - 1 Kijiko cha chai Vanilla - 1 Kijiko cha chai Hiliki zilizosagwa - 1 Kijiko cha chai Sukari ya laini ya unga (icing sugar) –robo Namna Ya Kutayarisha Na Kupika vunja mayai, tia sukari, hamira, baking powder, vanilla na hiliki kisha unapiga kwa kutumia mchapo wa kupigia keki. Unapiga mchanganyiko kwa muda wa dakika tano.Unatia siagi kwenye sufuria na unaiyayusha na kuipasha moto mpaka iwe moto ikisha unaimimina kwenye mchanganyiko na unapiga tena kwa dakika mbili tu.Unatia unga kwenye sinia au bakuli kubwa ikisha unamimina ule mchanganyiko kwenye unga na unaukanda kutumia mkono, mpaka ulainike.Ukiona unga mwingi basi ongeza maziwa kidogo mpaka uwe sawa, na ukiona unga mwepesi sana basi unaweza kuongeza unga kidogo pia mpaka ukae sawa mfano wa unga wa maandazi.Sukuma na ukate madonge kwa kutumia gilasi,Tumia kifuniko cha chupa kwa kukatia kiduara kidogo katikakti ya madonge. Ukimaliza kukata madonge yote, yaweke kidogo yavimbe kwa dakika 30 halafu teleka mafuta na uyachome.Ukitoa kwenye mafuta yachuje moto na kabla ya kupoa yawe moto moto ya chovye kwenye icing sugar na uhakikishe yote yameenea sukari juu.Ukimaliza tia kwenye sahani acha zipowe na zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Chapisha Maoni

0 Maoni

Ad Code

Responsive Advertisement