JINSI YA KUPIKA CHAPATI ZA MAJI
️MAHITAJI
1. Ngano ½ kilo
2. Mayai 3
3. Mafuta ¼ kikombe
kitunguu kikubwa kilichosagwa 1
4. Kitunguu Swaumu punje 4
5. Chumvi ½ kijiko au zaidi kulingana na matakwa yako
️JINSI YA KUPIKA CHAPATI
1. Chekecha unga wako vizuri weka katika bakuli safi.
2. Tia maji katika bakuli la unga na ukoroge mpaka upate uji wa wastani si mzito sana wala si mwepesi sana.
3. Ongeza mayai na chumvi endelea kukoroga.
4. Ongeza kitunguu swaumu na kitunguu maji. Injika kikaango chako jikoni subiri kipate moto.
5. Chota pawa moja mimina na tandaza kuzunguka kikaango subiri sekunde tano hadi kumi mpaka ikauke kisha geuza upande wa pili.
6. Tia mafuta huku ukigeuza na kuzungusha ili mafuta yaenee pande zote na ili chapati isiungue. Endelea kugeuza mpaka iwe rangi ya kahawia.
7. Hapo chapati zitakua tayari kwa kuliwa Fanya hivyo kwa chapati zote zilizobakia.
💥Chanzo : Facebook Group (JinsiYaKupika)
NB : PAGE YETU MASOMO YETU NI BURE KABISA LIKE & FOLLOW 👉 Jinsi Ya Kupika
0 Maoni