MTOTO ABAKA NA KULAWITI
#Mtwara:Ni tukio la kustaabisha ambapo jeshi la Polisi Mkoani Mtwara linamshikilia Mtoto mwenye umri wa miaka 14 ambaye ni Mkulima na Mkazi wa Kitongoji cha Chiano Kata ya Nalingu, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kwa tuhuma za kubaka na kulawiti Watoto wawili ambao ni Ndugu (Watoto wa Dada yake) ambao alikuwa anaachwa nao nyumbani kama Mlezi pindi Dada yake anapokwenda kufanya shughuli zake za kila siku za kujiingizia kipato.
Mama Mzazi wa Watatoto alipomuhoji Mdogo wake amekiri kufanya hivyo ambapo amesema Mtoto wa kike amembaka hadi akazoea na sasa anamuona kama Mke wake huku Mtoto wa kiume akiwa amemuingilia kwa siku tatu na alikuwa anafanya hivyo Mama yao anapokuwa mbali na nyumbani huku akiwatishia kuwa wakimwambia Mama yao atawapiga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Nicodemus Katembo amesema Mtoto aliyebakwa ni wa kike mwenye umri wa miaka saba na wa kiume wa miaka mitano amelawitiwa ambapo matukio hayo yametokea kuanzia October mosi hadi 15, mwaka huu, katika nyakati tofauti.

0 Maoni