#MICHEZO Kampuni inayojihusisha na michezo ya mieleka duniani maarufu kama "WWE" ina mpango wa kuandaa pambano kati ya nyota wa klabu ya Al Nassr Cristiano Ronaldo dhidi ya nguli wa mchezo huo wa mieleka John Cena kama sehemu ya uzinduzi wa mashindano ya mieleka yanayojulikana kama "Crown Jewel" ambayo yanatarajiwa kufanyika nchini Saudi Arabia Novemba 4 mwaka huu.
Unaambiwa baada ya kulipeleka soka Saudi Arabia, sasa ni zamu ya Ronaldo kuipeleka mieleka nchini humo.
Kati ya Ronaldo Vs John Cena unahisi nani atapigwa kama ngoma?
#WWE #CristianoRonaldoCR7 #EastAfricaTV
0 Maoni