-Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe ametozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kumkejeli na kumdhalilisha mwamuzi wa mchezo tajwa hapo juu, Tatu Malogo kupitia mitandao ya
kijamii
-Baada ya kumalizika kwa mchezo wa Singida Fountain Gate na Simba SC, Ali Kamwe aliweka chapisho (post) katika ukurasa wake binafsi wa mtandao wa kijamii wa Instagram, ambalo
lilikuwa na picha ya mwamuzi (Tatu Malogo) huku akiunganisha chapisho hilo na wimbo
wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Billnass uitwao Maokoto (neno lenye maana ya fedha kwa lugha isiyo rasmi), hali iliyoleta tafsiri ya kumhusisha mwamuzi huyo na masuala ya fedha ama rushwa.
Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 46:10 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Viongozi
0 Maoni