Shirikisho la soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa ndani wa mwaka ambapo Mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Fiston Mayele anayeichezea Pyramids FC ya Misri kwa sasa ameingia kwenye TATU BORA.
Mayele ameingia katika kipengele hicho baada ya kuwa na msimu mzuri na Yanga SC na kuifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika sambamba na kuibuka Mfungaji bora wa michuano hiyo.
Mayele anachuana winga wa Al Ahly, Percy Tau na mshambuliaji wa Mamelodi Sundowns Peter Shalulile.
0 Maoni