Goli la kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua dhidi ya Al Ahly kwenye mechi ya Jumamosi katika dimba la Mkapa, limetangazwa kuwa goli bora la wiki la michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1 na Ijumaa hii Yanga watakuwa nchini Ghana kucheza dhidi ya Medeama, mchezo wao wa tatu katika kundi D. #NestoShayoUPDATES
0 Maoni