JINSI YA KUPIKA UROJO
MAHITAJI YA UROJO: ili kuweza kupika urojo vizuri unatakiwa uwena vitu vifuatavyo:
Badia za (dengu au za kunde),kachori, chipsi za muhogo, mayai, mishkaki ya nyama.
NB: hivi vitu nilivyo viorodhesha unaweza ukaandaa kiasi unacho kutaka mwenyewe.
MAELEKEZO
-kama ni urojo wa embe basi zichemshe baada ya hapo zivuruge aidha kwa kijiko au kwa mkono (hakikisha kokwa ya embe isiingie wakati unazivuruga)
-chemsha maji kiasi kulingana na mahitaji yako mwenyewe (hakikisha maji yanachemka vizuri )
-weka unga wa ngano kwenye maji huku yanaendelea kuchemka koroga korogavizuri (hakikisha unga hufanyi madonge )
-baada ya hapo weka zile embe ulizo vuruga vizuri kisha endelea kukoroga vizuri
-hatua ya mwisho ni kuacha uchemke urojo wako baada ya kuchemka vizuri epua urojo wako kisha unaweza kuweka urojo kwenye kibakuli na kuweka yale mahitaji nilio orodhesha hapo juu.
NB: unaweza kuweka chumvi saizi unayo unayotaka au unaweza kuweka saladi kisha baada ya hapo unaweza kunywa urojo wako

0 Maoni