Ticker

6/recent/ticker-posts

Adsterra ad

JINSI YA KUPIKA WALI BIRIANI

JINSI YA KUPIKA WALI HUU UNAITWA JOLLOF RICE. MAARUFU SANAA KWENYE NNCHI ZA AFRICA YA KATI. MAHITAJI 1. Gram 240 ya mchele wowote ule 2. Kijiko 1 kikubwa cha chakula mafuta ya kupikia 3. Kijiko 1 kidogo cha chai binzali nyembamba 4. Kijiko 1 kidogo cha chai unga wa binzali 5. Kijiko ¼ kidogo cha chai unga wa kungu manga 6. Kitunguu 1 maji kikubwa 7. Gram 20 kitunguu swaumu 8. Gram 10 tangawizi 9. Gram 20 uyoga wowote ule 10. PiLiPiLi mbuzi mbichi 1 au 2 (sio lazima) 11. Kijiko 1 kikubwa cha chakula nyanya ya kopo 12. Nyanya 2 za kuiva kubwa chop chop 13. Carrot 1 kata vipande vidogo vidogo 14. Gram 60maharage mabichi 15. Gram 60 njegere mbichi 16. Gram 10 chumvi 16. Fungu 1 la majani ya giligilani JINSI YA KUPIKA Weka katika sufuria au kikaango mafuta ya kupikia kijiko 1 Kisha weka cumin seeds zikisha pata moto zikapasuka weka kitunguu maji, tangawizi, kitunguu swaumu na pili pili mbuzi vyote viwe umekata chop chop na uendelee kukaanga. Kisha ongeza carrots koroga na kisha weka chumvi. Kisha weka tomato paste/nyanya ya kuiva uliyokata vipande vidogo pamoja na curry powder. Pika mapka uhakikishe nyanya imeiva. Kisha weka wali. Kaanga wali wako kwa dakika 3 hakikisha moto ni wa wastani. Kisha ongeza maji 480 gram, onja chumvi kama haitoshi ongeza tena kidogo,Kisha funika kikaango chako au sufuria na pika mpaka maji yakauke kabisa Kisha weka maharage mabichi na njegere na uyoga hakikisha ulisha zichemsha kabla kama ni mbichi basi unatakiwa uzipike wakati unaweka mchele mwanzo kabisa ili nazo ziweze kuiva. Hakikisha unakoroga vizuri kabisa mpaka inachanganyika saafi, kisha ongeza unga wa kungu manga pika kwa dakika 5 ili ladha ichanganyike safi kabisa kati ya wali wako na mboga majani Pia badala ya uyoga unaweza tumia nyama ya ngombe au nyama ya kuku na pia hata prawns lakini inabidi uzikaange nyama hizi wakati unaweka mchele ili ziive pamoja na unatakiw aukate vipande vidogo vidogo sana iwe rahisi kuiva. NB ; HILI SOMO KUELEWA ITAKUWA NGUMU KWAKUWA HIKI CHAKULA SIO CHA ASILI YETU USIJALI KWA MASOMO MENGINE LIKE & FOLLOW 👉 Jinsi Ya Kupika MASOMO YETU NI BURE KABISA.

Chapisha Maoni

0 Maoni

Ad Code

Responsive Advertisement