mwaka 2020 MOHBAD alijiunga na label ya muziki iitwayo Marlian records ambayo inasimamiwa na star wa muziki Naira marley nchini nigeria
Mohbad aliachia EP yake ikaenda viral na watu wengi waliguswa na kipaji kikubwa alichokuwa nacho ,ila baada ya miaka miwili alitangaza kuachana na Label ya Naira marley kutokana na sababu nyingi hasa ugomvi wa siri siri na boss wake
Baada ya hapo maisha ya mohbad yalibadirika sana na mpaka kupelekea kifo chake tarehe 12 mwezi huu
Nini kipo nyuma ya pazia kuhusu kifo chake
inasemekana kifo chake sio cha kawaida bali ameuawa ,shutuma hizo zinamlenga boss wake Naira marley
Mohbad aliwahi toa malalamiko kuwa anatishiwa usalama wa maisha na boss wake ,lakini pia kuna baadhi ya video (footage) zilionekana Jinsi Mohbad anavyopigwa na kundi la wahuni, mkuu wa kundi la wahuni anaitwa Sam rally ambaye ni rafiki mkubwa wa Naira marley
kabla ya kifo chake,alionekana akiongea kwa uchungu hospital akidai kuwa mtu wa mwisho kuonana nae alikuwa ni Naira marley ,Mohbad alisema kuwa siku hiyo kuna dawa aliwekewa ambazo zilimuathiri mpaka afya yake ikawa inadhoofika taratibu
baada ya mohbad kufariki alizikwa haraka sana ,kinachonisikitisha mimi amezikwa kama mnyama ,jeneza alilowekwa lilikuwa halitoshi hivyo walivunja shingo yake ili atoshe tu !
uchunguzi unaendelea kufanyika juu ya kifo hicho kwani maiti imefukuliwa ili ipimwe ,kwa sasa kila mtu anaongea lake wengine wanasema alizikwa akiwa mzima kwasababu kwenye jeneza lake walikuta damu ,wengine wanasema alikufa kwa msongo wa mawazo (stress)

0 Maoni