Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mh Juma Chikoka ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuwalinda, kuwatunza na kuwapa nafasi wanafunzi wa kike wapate fursa ya kusoma ili watimize ndoto na malengo yao.
Mh Dc alisema yapo matukio kama mimba za utotoni, ubakaji, ukatili na unyanyasaji wa watoto ufikie mwisho na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote wataobainika kutaka kukatisha ndo za watoto hawa.
Mh Dc Chikoka alizungumza hayo wakati wa ufunguzi wa harambee ya Ujenzi wa bweni la shule ya Sekondari ya wasichana ya Rorya Girls ambapo wananchi na viongozi mbalimbali wameanzisha Ujenzi huo.
Dc Chikoka alisisitiza kwamba Imani ya Serikali ya wilaya ni kwamba ukiwekeza kwenye elimu ya mtoto wa kike, umewekeza kwa Jamii.
0 Maoni