Tangu ligi kuu Tanzania bara hajawahi kutokea kipa mwenye quality kubwa kama Djidui Diarra kipa wa Yanga SC na timu ya taifa ya Mali namna anavyodaka udakaji wake wa kisasa.
Katika Misimu miwili ameshinda tuzo ya kipa Bora kwa kumpora Tanzania one Aishi Manula ambaye alijimilikisha tuzo kwa kuchukua mara sita bila kupata mtu wa kumchallange lakini pia ameshinda tuzo ya kipa Bora kwenye fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika msimu uliopita dhidi ya Usm Alger.
Kupitia orodha iliyotolewa na CAF kipa huyu raia wa Mali ameingia kwenye vipengele viwili kipa Bora wa mwaka wa Afrika na mchezaji Bora wa klabu lakini katika kipengele Cha kipa Bora ana shindana na majina makubwa yanayocheza katika klabu kubwa barani ulaya na Uarabuni kama Andre Onana kutoka Man utd,Edouard Mendy,pamoja na makioa kutoka vilabu vukibwa Afrika Ronwen Williams pamoja na Kipa wa Al Ahly Mohammed El Shanawy hiyo ni ishara ya ubora mkubwa alikuwa nao kipa Huyo wa timu ya taifa ya Mali.
NB: Makipa wote katika ligi yetu wanamtazama Diarra kasoro Aishi Manula.
Credit by @isayah_dede18

0 Maoni