Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Samatta amedai kufurahia goli lake la kwanza akiwa na Klabu yake mpya ya Paok FC.
“Alama 3 nyingine na furaha ya goli la kwamza kwa timu,”- Ameandika Samatta
Staa huyo wa Taifa Stars, Samatta amefunga goli hilo dakika ya 55 kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Volos.
Paok FC inashika nafasi ya pili kwenye Msimamo wa Ligi ya Ugiriki
0 Maoni